top of page

Upendo- Paul Clement
Verse 1
Unazijua siri zangu, Lakini hukumwambia mtu,
Kuwa niliiba, Kile nilifanya,
Pale nilisema uongo
Unazijua siri zangu, Lakini hukumwambia mtu,
Kuwa niliiba, Kile nilifanya,
Pale nilisema uongo
Chorus
Unazijua siri zangu, Lakini umezificha,
Ukiamua uziseme, Nitaaibika,
Unazijua siri zangu, Lakini umezificha,
Umeamua unisitiri, Ndivyo ulivyopenda.
Verse 2
Unaujua undani wangu, Lakini hukumwambia mtu,
Kuwa ni mdhaifu, Tena ni mchafu,
Umenifunika tu
Unaujua moyo wangu, Unayajua mawazo yake,
Si mawazo mema, Yasiopendeza,
Umenifunika tu
Chorus
Unazijua siri zangu, Lakini umezificha,
Ukiamua uziseme, Nitaaibika,
Unazijua siri zangu, Lakini umezificha,
Umeamua unisitiri, Ndivyo ulivyopenda.
bottom of page